Home Uncategorized YANGA YAWATAKA MASHABIKI KUSAHAU MATOKEO YA 4G MAISHA LAZIMA YAENDELEE

YANGA YAWATAKA MASHABIKI KUSAHAU MATOKEO YA 4G MAISHA LAZIMA YAENDELEE


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa kwa sasa ni muhimu mashabiki kusahau kuhusu matokeo ya mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba kwa kuwa maisha lazima yaendelee.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kila mmoja aliona kilichotokea Uwanja wa Taifa hivyo benchi la ufundi litafanyia kazi makosa.

Kesho, Julai 15, Yanga inacheza mchezo wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Taifa dhidi ya Singida United ambayo tayari imeshahuka daraja baada ya kucheza mechi 34 na kushinda tatu ikiwa na sare sita, imefungwa jumla ya mechi 25.

Singida United iliyo nafasi ya 20 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya tatu ikiwa na hasira ya kupokea kichapo cha mabao 4-1 mbele ya watani zao Simba, Julai 12 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali.

Yanga pia inakutana na Singida United yenye hasira za kupoteza mchezo wake uliopita mbele ya KMC kwa kufungwa mabao 2-0.

“Matokeo yameshatokea hatuwezi kubadili, kwa sasa tunatazama mechi zilizobaki namna gani tutapata matokeo chanya, tuna muda wa kujipanga na kupata matokeo mazuri wakati ujao.

“Mashabiki waendelee kutupa sapoti tupo imara na Yanga ni timu kubwa na ina nguvu, bado tunayo nafasi ya kurekebisha makosa yetu,” amesema.

SOMA NA HII  KIPA AGOMEA MKATABA SIMBA / KABWILI SAMATTA MFANO WA KUIGWA - VIDEO