NYOTA wa Yanga, Feisal Salum amesema kuwa iwapo Simba ama Azam watahitaji huduma yake hana tatizo nao kwa kuwa kazi yake ni mpira hana chaguo iwapo utaratibu utafuatwa.
Feisal amekuwa kwenye ubora wake ndani ya Yanga akiwa na uwezo wa kufunga pamoja na kutibua mipango ya wapinzani wake.
Kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho walipokutana na Simba wakati wakipoteza kwa kufungwa mabao 4-1 alimtungua Aishi Manula kwa pasi ya Jonas Mkude.
Pia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mbele ya Mwadui FC wakati wakilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Taifa alimtungua mlinda mlango wa Mwadui FC, Mussa Mbissa kwa pasi ya Mrisho Ngassa.
“Mimi ni mchezaji na ikitokea nimepewa ofa iwe Simba ama Azam FC sina tatizo nitafanya kazi ila muhimu utaratibu kufuatwa nitafanya kazi,” amesema.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.