Mchezaji wa Taifa StarsSimon Msuva baada ya kuisaidia Taifa Stars kwa kufunga goli 1-0 dhidi ya Uganda wamerejea nchini leo
wakitokea Misri walipocheza mchezo huo wa kuwania AFCON 2023 nchini Ivory Coast.
Msuva baada ya kurejea nchini wengi walitaka kufahamu amepokeaje ahadi ya Rais Samia aliyoitoa ya kutoa zawadi ya Tsh milioni 10 kwa kila goli watakalofunga.
“Kwa uwezo wa Mungu AFCON tutakwenda, kuhusu ahadi
tumeipokea vizuri kama na hatuwezi kumuangusha,” amesema Msuva.