UONGOZI wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba umesema kuwa kushika kwao nafasi ya pili kwenye msimamo ni heshima kubwa hasa kwa upande wa rekodi.
Azam ipo nafasi ya tatu ikiwa ina pointi 66 inapambania nafasi ya pili ambayo ipo mikononi mwa Yanga yenye pointi 69 jambo linaloongeza ushindani wa nafasi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thabit Zakaria, Ofisa Habari wa Azam FC, amesema kuwa malengo ya klabu ni kuona yanatimia kwa kumaliza kwenye nafasi ya pili ambayo kwao ni sehemu ya rekodi.
“Tulianza na malengo ya kufikiria ubingwa ukapotea, tukaongeza malengo ya kuwa nafasi ya pili sababu kubwa kuhitaji nafasi hii ni heshima pamoja na rekodi kwani kuna wakati unatazama msimu fulani ukiwa wapi na ulifanya nini kwetu ni mafanikio pia.
“Kitu pekee kilichobaki kwa sasa kwetu ni kuangalia makosa yetu na kupambana kushinda mechi zetu kwani tuna mchezo na Mbeya City nao ni mgumu hivyo bado tunasubiri kuona mambo yatakuaje,” amesema Zakaria.
Kwenye mchezo wa leo mbele ya Mbeya City itakosa huduma ya beki Nicolas Wadada ambaye ana kadi tatu za njano.