Home Uncategorized AZAM FC YAPANIA KUFANYA KWELI MBELE YA SIMBA LEO TAIFA

AZAM FC YAPANIA KUFANYA KWELI MBELE YA SIMBA LEO TAIFA


MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho, Azam FC wamesema kuwa hakuna namna yoyote ile itakayowazuia kulitwaa taji hilo kwa kuwa wamejipanga kuweza kufikia malengo yao.
Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba, ilitwaa taji hilo kwa kuitungua Lipuli FC bao 1-0, bao lililjazwa kimaina na mshambuliaji wao namba moja Obrey Chirwa kwa pasi ndefu ya mlinda mlango Razack Abarola.
Itamenyana na Simba, leo, Julai Mosi Uwanja wa Taifa hatua ya robo fainali ikipenya hapo itakutana na Yanga ambaye alishinda mbele ya Kagera Sugar mabao 2-1.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa ila wapo tayari kwa kuwa maandalizi yalianza mapema.
“Tulikuwa tunafanya maandalizi ya mambo mawili kwenye Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho, tunataka kulitwaa kombe hili kwa mara nyingine ili kuwakilisha nchi kimataifa kwa kuwa tulifanya hivyo msimu uliopita tunahitaji kurudi tena,” amesema Thabit.
 Azam FC inautazama mchezo wa leo kwa jicho la kipekee kwa kuwa imeshapoteza nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kupoteza nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.
Simba itaingia uwanjani ikiwa haina cha kupoteza kwa kuwa imeshabeba taji la Ligi Kuu Bara na wachezaji ila itaingia kwa kutafuta heshima uwanjani.
SOMA NA HII  KAGERA SUGAR: HAKUNA TIMU NINAYOIGOPA, NIKIFUNGWA NAFUNGWA KWELI, NIKIFUNGA NAFUNGA