Home Uncategorized BAADA YA KUICHAPA YANGA JANA..BOCCO NA KAGERE WABEBA TUZO

BAADA YA KUICHAPA YANGA JANA..BOCCO NA KAGERE WABEBA TUZO

MASTAA wawili wa Simba, Meddie Kagere na John Bocco wameula kwenye tuzo za wachezaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Machi na Juni.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Meddie Kagere amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Machi msimu wa 2019/2020.

Ameibuka kidedea kwa kuwashinda wenzake Paulo Nonga wa Lipuli na Never Tigere wa Azam FC alioingia nao fainali.

Kwa mwezi huo Kagere aliiongoza timu yake kushinda michezo mitatu na kupoteza moja ikibaki kileleni mwa msimamo wa ligi,  huku Kagere akifunga mabao matano, ambapo Simba iliifunga Azam FC mabao 3-2, ikaifunga Singida United mabao 8-0 na ikaifunga KMC mabao 2-0 na ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Yanga.

Bocco yeye amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Juni baada ya kuwashinda wenzake Atupele Green wa Biashara United na Martin Kiggi wa Alliance FC alioingia nao fainali.

Bocco alikuwa na kiwango bora akiisaidia Simba kushinda michezo miwili na kutoka sare miwili ikiendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu , akipachika nyavuni mabao matatu katika michezo minne aliyocheza. Simba iliifunga Mwadui mabao 3-0, ikaizamisha Mbeya City mabao 2-0 ikatoka sare na Ruvu Shooting mabao 1-1 na ikatoka 0-0 na Prisons.

SOMA NA HII  MOLINGA SASA KUONGEZEWA MKATABA YANGA