Home Uncategorized MTIBWA SUGAR WAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA

MTIBWA SUGAR WAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA


UONGOZI wa Mtibwa Sugar, umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya yanga unaoatarajiwa kuchezwa Julai 22, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mtibwa Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila kwa msimu wa 2019/20 mambo yamekuwa magumu kwao tofauti na msimu uliopita wa 2018/19 kwa kupata matokeo ya kususua zaidi.

Kwa sasa ipo nafasi ya 14 ikiwa imejikusanyia pointi 41 baada ya kucheza mechi 36 inakutana na Yanga ambayo ipo nafasi ya pili na pointi 68.

Mchezo wao uliopita wametoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya KMC, Uwanja wa Gairo wanakutana na Yanga iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mwadui FC Uwanja wa Taifa.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa ni mchezo mgumu kwao ila watapambana kupata matokeo chanya ambayo yatawafanya wabaki ndani ya ligi.

“Tunajua ni mchezo mgumu dhidi ya Yanga ila hakuna namna lazima tupambane tupate matokeo kama ambavyo tumekubaliana kwa pamoja, kupoteza mbele ya KMC kumetufanya tuongeze juhudi zaidi, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  AZAM FC YAANZA KUJIWEKA MGUU SAWA KWA AJILI YA KUMENYANA NA KAGERA SUGAR