Home Uncategorized YANGA WATOA TAMKO BAADA YA KUPOKEA KICHAPO CHA 4G MBELE YA SIMBA

YANGA WATOA TAMKO BAADA YA KUPOKEA KICHAPO CHA 4G MBELE YA SIMBA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa haikuwa bahati yao jana kushinda mbele ya Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kwa kuchapwa mabao 4-1 mbele ya Simba.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa ulikuwa na ushindani mkubwa  ambapo Simba walianza kwa kasi kipindi cha kwanza na kipindi cha pili Yanga nao waliweza kubadili upepo wa mchezo.

Simba walipata bao la kwanza dakika ya 21 kupitia kwa Gerson Fraga ambalo lilidumu mpaka wakati wa mapumziko na kipindi cha pili Simba ilifunga mabao matatu.

Alianza Clatous Chama dakika ya 50, Miquissone dakika ya 52 na lile la nne lilifungwa na mzawa Mzamiru Yassin na lile la Yanga likifungwa na kiungo mzawa, Feisal Salum,’Fei Toto’.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa makosa yao yamewagharimu hivyo wanajipanga kwa ajili ya msimu ujao.

“Tumeshindwa kwenye mchezo wetu hilo lipo wazi lakini haina maana kwamba msimu ujao tutashindwa kufanya vizuri.

“Kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya msimu ujao ili kuwa bora zaidi kwani kila kitu ni mipango tunaamini kuwa kila kitu kitakuwa sawa, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  ISHU YA AUBAMEYANG KUTAJWA CHELSEA YAZUA MSHTUKO