Uncategorized

CHAMA ASEPA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA KOMBE LA SHIRIKISHO

admin August 2, 2020 3:47 pm

CLATOUS Chama nyota wa kikosi cha Simba leo amekabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano ya Kombe la Shirikisho. 

Simba imetwaa taji mbele ya Namungo FC kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa kibabe uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela,  Sumbawanga. 

Mabao ya Simba yalifungwa na Luis Miqussone na John Bocco na lile la Namungo lilifungwa na Edward Manyama.

Chama ndani ya Simba ni kinara wa kutupia mabao akiwa nayo manne na pasi tatu za mabao.

Chama amesema:”Furaha kubwa katika hili kwa kuwa ilikuwa ni kazi ngumu ila tumefanikiwa kwa kuwa sisi sote ni timu moja.”

LYANGA AJIFUNGA MIAKA MIWILI AZAM FC SIMBA YAWEKA REKODI NDANI YA MSIMU WA 2019/20, YAKUSANYA MATAJI MATATU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply