Home Uncategorized KIPA NAMBA MBILI WA SIMBA, BENO KAKOLANYA ATAJWA KUIBUKIA AZAM FC

KIPA NAMBA MBILI WA SIMBA, BENO KAKOLANYA ATAJWA KUIBUKIA AZAM FC


TETESI za usajili katika kuelekea msimu ujao, zinasema kuwa upo uwezekano mkubwa wa kipa namba mbili wa SimbaBeno Kakolanya kujiunga na Azam FC katika msimu ujao.
Kipa huyo tangu amejiunga na Simba msimu huu uliomalizika 2019/2020, ameonekana kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Kakolanya ikumbukwe kuwa hivi karibuni alitofautiana na kocha wake wa makipa, Mohammed Mwalami baada ya kumuondoa kwenye msafara wa timu hiyo uliokwenda mkoani Tanga kucheza mchezo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union Julai 23 kwa kile alichodai ana majeraha wakati yeye ni mzima.

Ila kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, na Simba kutoshana nguvu ya bila kufungana alikaa kwenye lango Kakolanya.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, Kakolanya anatajwa kwenda Azam kuchukua nafasi ya kipa Mghana, Razak Abarola ambaye ameachwa na timu hiyo.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kipa mwenyewe Kakolanya ndiye aliyeomba kuondoka hapo Simba na kwenda Azam baada ya kuonekana hana maelewano mazuri na kocha wake wa makipa, pia kupoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.
“Yapo mazungumzo ya siri yanafanywa kati ya uongozi wa Simba na Azam waliomuomba kipa huyo kwenda kuichezea timu hiyo huku wakipanga kununua mkataba wake wa mwaka mmoja alioubakisha Kakolanya.
“Kakolanya anaonekana hana furaha tangu alipojiunga na timu hiyo, hiyo ni baada ya kuonekana kushindwa kumtoa Manula katika kikosi cha kwanza kabla ya kuomba kuondoka mwenyewe.
“Kitendo cha yeye kutopata nafasi ya kucheza kimemfanya akose furaha ndani ya timu hiyo, hivyo akaona ni bora akaondoka hapo na kwenda kwingine kucheza,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Kakolanya ambaye alikuwa kwenye maandalizi ya mchezo wa Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Namungo FC kwa njia ya simu kuzungumzia hilo, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.
SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR INA MKAKATI WA KUJENGA BONGE MOJA YA UWANJA, HAYA HAPA MAFANIKIO YAO