MABINGWA wa Ligi Kuu England, Liverpool wamekutana na kizingiti kutoka Norwich City kumpata beki Jamal Lewis ili aibukie ndani ya Uwanja wa Anfield hasa kwa upande wa dau.
Lewis mwenye miaka 22 anatajwa kuingia kwenye rada za Liverpool inayonolewa na Jurgen Klopp ambaye amekuwa akivutiwa na beki huyo.
Dau ambalo Liverpool wameliweka mezani ni pauni milioni 10 huku Norwich wakihitaji kupewa pauni milioni 20 jambo ambalo linawafanya Liverpool kuwa kwenye ugumu wa kuipata saini ya beki huyo.
Malengo makubwa ya Klopp ni kumpata msaidizi wa beki wake Andy Robertson ili awe na kikosi kipana ambacho kitaendeleza ushindani ndani ya Ligi Kuu ya England ambayo ina ushindani mkubwa.
Norwich ipo tayari kumuuza Lewis ila kikubwa wanataka thamani kubwa ya beki huyo kwenye ada ya dau la usajili jambo ambalo limekuwa kizingiti kwa Liverpool.
Tayari Liverpool imeshakamilisha dili la kumuuza beki wao Dejan Lovren ambaye yupo Zenit St Petersburg kwa dau la pauni milioni 10 hivyo uhitaji wao wa kumpata Lewis ili awe mbadala wa nyota huyo kwenye nafasi hiyo ni mkubwa.