UONGOZI wa Simba umesema kuwa suala la mchezaji wao Clatous Chama kutajwa kujiunga na watani zao wa jadi Yanga hazina ukweli.
Imekuwa ikiripotiwa kuwa baada ya Yanga kumvuta ndani ya Yaga Senzo Mbatha aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba imeanza hesabu za kumvuta ndani ya kikosi kiungo wao bora, Chama.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Simba haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo kwa kuwa ina mkataba naye na ina malengo.
“Chama ana mkataba na Simba hadi Julai 2021, Simba haiwezi kumuuza au kumuachia mchezaji ambae tuna malengo nae.
“Najua viongozi wao wanataka kuwaongopea watu wao ili kutoa droo na issue ya Morrison,” amesema.
Clatous Chama amesema kuwa masuala ya mitandao hayana ukweli yeye bado ana mkataba na timu yake ya Simba.