Uncategorized

ISHU YA MORRISON YAKWAMA TENA LEO, SASA NI MPAKA KESHO

admin August 11, 2020 2:47 pm

 MWENYEKITI wa Kamatiya Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF), Elias Mwanjala amesema kesi ya Bernard Morrison itaendelea kuskilizwa kesho.


Kiungo wa Yanga, Morrison alikuwa na mvutano mkubwa na klabu ya yake kuhusu sakata la mkataba ambapo yeye anadai kwamba ana dili la miezi sita ambalo limekwisha huku Yanga ikieleza kuwa ana dili la miaka miwili.

Sakata lake leo ni siku ya pili ambapo lilianza kusikilizwa jana, Agosti 10 na leo Agosti 11 pia limeskilizwa na hakuna majibu ambayo yametolewa.

Mwanjala amesema kuwa kuna document  moja haijakamilika kwa pande zote mbili ya Yanga na Morrison  na pande zote zimesema jioni ya leo watazileta.

“Kuna nyaraka ambazo hazijakamilika kwa pande zote mbili, moja ya Yanga na moja ya Morrison jambo ambalo limefanya tushindwe kutoa maamuzi.

“Kesho zitakabidhiwa kwa kamati ambapo kikao kitaanza kesho saa 4 asubuhi kufikia saa saba na nusu kesho kikao kitakuwa kimekwisha na watatoa maamuzi juu ya kesi hiyo.”

Morrison Agosti 8 kesi yake ikiwa bado haijatolewa hukumu alitambulishwa na watani wa jadi Simba huku ikielezwa kuwa amesaini kandarasi ya miaka miwili jambo linaloongeza mvutano wa uhalali wake.

  
RASMI YANGA YAMALIZANA NA MBUKINAFASO AZAM FC WAJIPA MATUMAINI YA KUFANYA MAKUBWA MSIMU UJAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply