TAARIFA za uhakika zinaeleza kuwa Yanga imemaliza na AS Vita na kumsajili mshambuliaji kinda wa AS Vita ya DRC, Tuisila Kisinda.
Shughuli hiyo imefanyika jijini Kinshasa, DRC na Yanga imewakilishwa na Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa uwekezaji wa Kampuni ya GSM.
Mtu wa karibu na Kocha Mkuu wa AS Vita amesema kuwa sababu kubwa iliyompeleka kigogo huyo wa GSM ni kumalizana na wachezaji anaowahitaji kwa ajili ya kuimarisha nguvu ndani ya kikosi cha Yanga.
“Amekuja kiongozi kutoka Yanga ambaye ni mkubwa na ameongea na Kocha Mkuu wa AS Vita ili kupata wachezaji wawili kutoka Congo, hivyo ninaamini kwa kuwa wamekuwa na ukaribu kwa muda na wamezungumza mengi ni suala la kusubiri tu,” ilieleza taarifa hiyo.