Home Uncategorized ISHU YA HAJI MANARA KUACHIA NGAZI SIMBA IPO HIVI

ISHU YA HAJI MANARA KUACHIA NGAZI SIMBA IPO HIVI

 

OFISA Habari wa Simba, Haji Manara leo Agosti 19, 2020 amefuta kauli yake ya kustaafu nafasi yake ya ndani ya Klabu ya Simba.

Agosti 16, Manara alisema kuwa anampango wa kuachia ngazi kwenye masuala ya uongozi ndani ya Simba kwa kuwa anasumbuliwa na matatizo ya kiafya lakini angebaki kuwa mshauri na muhamasishaji wa Klabu ya Simba kwa kuwa ni mwanachama.
Leo, Agosti 19 Manara amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuondoka ndani ya Simba kwa kuwa amethibitishiwa na wataalamu wa afya kuwa yupo fiti.

“Jana Agosti 18, nimepimwa na madaktari na wameniambia kuwa nipo fiti, kuanzia kwenye moyo, mapafu nipo vema na ninaamini kwamba nitaendelea kuwepo ndani ya Klabu ya Simba.
“Bado nipo ndani ya Simba kwa sasa, ninaomba taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa awali kuwa nitaondoka ndani ya Simba zipuuzwe,” amesema.
SOMA NA HII  SIMBA IPO KAMILI GADO KUVAANA NA MBEYA CITY KESHO