Home Uncategorized KICHAPO CHA MABAO 8-2 KINAWAFIKIRISHA KUSEPA MASTAA WENGI BARCELONA

KICHAPO CHA MABAO 8-2 KINAWAFIKIRISHA KUSEPA MASTAA WENGI BARCELONA

 LUIS Suarez, staa wa Klabu ya Barcelona ni miongoni mwa nyota wanaotajwa kuwa kwenye mpango wa kusepa ndani ya klabu hiyo msimu ujao baada ya kupoteza kwa kichapo kikubwa cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munich.

Barcelona ilipokea kichapo hicho kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali na kushuhudia Bayern Munich ikitinga hatua ya nusu fainali ambapo leo itacheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Lyon utakaopigwa nchini Ureno.

Tayari PSG ishajikatia tiketi ya kushiriki fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Leipzing usiku wa kuamkia leo.

Fainali inatarajiwa kuchezwa Agosti 23, Uwanja wa Estadio do Sport Lisbon.

Pete Jenson, mwandishi wa Daily Mail amesema kuwa kuna mpasuko mkubwa wa nafsi za nyota wengi ndani ya Klabu ya Barcelona jambo linalowafanya wengi wafikirie kuondoka.

Mbali na Suarez pia staa wao namba moja ambaye alitupia jumla ya mabao 25 ndani ya La Liga, Lionel Messi naye anatajwa kupiga hesabu za kutimka ndani ya kikosi hicho.

SOMA NA HII  WALIOPIGWA MBILI NA SIMBA WASAJILI WAPYA SITA