Home Uncategorized NAMUNGO FC YAIPIGIA HESABU SIMBA NGAO YA JAMII

NAMUNGO FC YAIPIGIA HESABU SIMBA NGAO YA JAMII

 


KOCHA Mkuu wa Namungo, Hitimana Thiery amewaahidi mashabiki wa timu hiyo kuwa watafanya vizuri kwenye mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

 

Mtanange huo ni maalum kwa ajili ya ufunguzi wa msimu wa 2020/21 ambapo unatarajiwa kupigwa Agosti 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha


Akizungumza na Saleh Jembe, Hitimana amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanaamini watakutana na timu kubwa hivyo watapambana.


 â€śWachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Simba.Wanatambua kwamba haitakuwa kazi rahisi ila wapo tayari hivyo kilichobaki ni wakati kukamilisha yale ambayo wamejifunza.


“Tunacheza na timu kubwa, wana taji la ligi pia tulikutana kwenye Kombe la Shirikisho tukapoteza hivyo yote ninakumbuka bado sijasahau” amesema.

SOMA NA HII  WAMISRI WAMKOMALIA KICHUYA KONA WA SIMBA, FIFA KUSHUSHA RUNGU KWA SIMBA