Home Uncategorized SABABU YA YANGA KUTOCHEZA NA SEVILLA KILELE CHA WANANCHI HII HAPA

SABABU YA YANGA KUTOCHEZA NA SEVILLA KILELE CHA WANANCHI HII HAPA

 

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mpango mkubwa kwenye kilele cha Wiki ya Wanachi, Agosti 30 ilikuwa ni kucheza dhidi ya Klabu ya Sevila ambao ni mabingwa wa Kombe la Europa League baada ya kuwatungua mabao 3-2 Inter Milan kwenye fainali iliyochezwa usiku wa kuamkia leo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa walikuwa wanahitaji kucheza na Sevilla siku ya kilele kwa kuwa  wanaushirikiano nao mkubwa ila mipango imekwama.

“Timu yetu ya kwanza ambayo ilikuwa ni chaguo letu kucheza nao ilikuwa ni Sevilla kwa kuwa tupo nao kwenye ushirikiano lakini mambo yamekuwa magumu kwa kuwa janga la Virusi vya Corona limevuruga mambo mengi na imekuwa ngumu kwa sasa kupata timu ambazo zinaweza kuwa huru kwenye kusafiri.

“Tuna uwezo kwa kuwa Yanga ni timu kubwa na inafanya mambo makubwa, tunaongoza kwa kuwa na mataji mengi hivyo hatuna cha kuhofia. Kwa kuwa tumeshindwa kuwapata Sevilla bado tunaendelea kufanya mawasiliano na timu nyingine ili tuweze kucheza mchezo mzuri wa kimataifa Uwanja wa Mkapa.

“Tutaitangaza timu ambayo tutacheza nayo hivi karibuni ila kwa sasa tumetuma barua pia kwa Rayon Sports ya Burundi nayo ni timu kubwa mipango ikikamilika kila kitu kitatangazwa,” amesema.

SOMA NA HII  WINGA MPYA WA YANGA KUANZA MAJUKUMU YAKE