UONGOZI wa Simba umesema kuwa Mtendaji Mkuu mpya ndani ya Simba (CEO), atakuwa ni Barbara Gonzalez ambaye atarithi kiti cha Senzo Mbatha.
Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohamed Dewji amesema kuwa ni makubaliano ya uongozi jana ambapo walikuwa na kikao cha Bodi ya Wakurugenzi, Septemba 4.
Anakuwa CEO wa kwanza wa kike ndani ya Bongo kwa msimu wa 2020/21 kuiongoza klabu hiyo yenye maskani yake Msimbazi.
Mbatha yupo ndani ya kikosi cha Yanga ambapo aliibukia huko muda mfupi baada ya kujiuzulu ndani ya Simba.