MANE AWAMALIZA CHELSEA DARAJANI JUMLAJUMLA
JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa wachezaji wake walipambana muda wote ndani ya uwanja mbele ya Chelsea wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Chelsea, usiku wa kuamkia leo.
Mchezo huo wa Ligi Kuu England ulikuwa ni wa pili kwa Liverpool kushinda baada ya kuanza kuichapa Leeds mabao 4-0, ulichezwa Uwanja wa Stamford Bridge ilipo ngome ya Chelsea inayonolewa na Frank Lampard.
Mabao ya ushindi kwa Liverpool yalipatikana dakika ya 50 na 54 mtupiaji akiwa ni Sadio Mane, raia wa Senegal ambaye aliwamaliza kabisa Chelsea wakiwa darajani.
Chelsea ilikuwa ikipewa nafasi ya kufanya vizuri kutokana na usajili wao makini lakini kadi nyekundu aliyoonyeshwa beki wao Andreas Christensene dakika ya 44 baada ya kumchezea faulo Mane iliwatoa kwenye ramani.
Kipa wa Liverpool, Allison Becker aliipangua penalti iliyopigwa na Joginho dakika ya 75 na kuwafanya Liverpool kusepa mazima na pointi tatu bila nyavu zao kutikiswa.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.