AZAM FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Aristica Cioaba raia wa Romania imeweka rekodi yake kwa msimu wa 2020/21 baada ya kucheza mechi nne ambazo ni dakika 360 bila kupoteza hata mchezo mmoja mfululizo.
Ilianza kufungua pazia leka la ligi mbele ya Polisi Tanzania wakati ikishinda bao 1-0 na ilishinda mabao 2-0 mbele ya Coastal Union zote zilichezwa Uwanja wa Azam Complex.
Mechi zake mbili ugenini imeshinda zote ilikuwa mbele ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine na ilishinda pia mbele ya Tanzania Prisons kwa bao 1-0 Uwanja wa Nelson Mandela.
David Kissu kipa namba moja wa Azam FC ameweza kuandika rekodi matata baada ya kucheza mechi zote nne bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa ndani ya dakikza 360.
Ipo nafasi ya kwanza ikiwa na jumla ya pointi 12 na imefunga mabao matano na kinara wao ni Prince Dube mwenye mabao matatu huku ikifuatiwa na Simba iliyo nafasi ya pili na ina pointi 10 kibindoni.