JUMA Mwambusi, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa kwa namna kikosi ambavyo kinatengenezwa kwa sasa kuna timu itapigwa mabao 10 ndani ya dakika 90.
Yanga jana Septemba 27 iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Bao pekee la ushindi lilifungwa na beki kisiki wa Yanga, Lamine Moro dakika ya 61 akimalizia mpira wa pigo la kona lililopigwa na Carlos Carinhos.
Mwambusi amesema:”Tunazidi kukijenga kikosi kwa sasa na kwa namna ambavyo tunakuja hivi kuna timu itafungwa mabao 10,8 na kuendelea.
“Kikubwa ambacho tunakihitaji ndani ya uwanja ni pointi tatu hivyo kwa sasa mashabiki waendelee kutupa sapoti mambo mazuri yanakuja.” amesema.
Yanga ipo nafasi ya tatu ina pointi 10 kibindoni baada ya kucheza mechi nne sawa na watani zao wa jadi Simba ambao wapo nafasi ya pili wakitofautiana kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Simba imefunga mabao 10 na Yanga imefunga mabao manne ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21.Kinara ni Azam FC ambaye hajapoteza mchezo hata mmoja kati ya minne akiwa na pointi 12 na mabao matano kibindoni.