Habari za michezo
SIMBA NA YAHYA MBEGU MPAKA KIELEWEKE
Staff Desk
October 18, 2023
3:55 pm
Taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Simba zinasema kuwa, viongozi wa timu hiyo bado wanaendelea kufuatilia kwa karibu Kiwango cha Yahya Mbegu wa Singida Fountain Gates.
Ikumbukwe kuwa Simba hapo awali walikuwa wakihitaji huduma ya beki huyo wakushoto lakini Yeye aliamua Kujiunga na Singida Fountain Gate mwanzoni mwa msimu huu.
Mbegu anatazamiwa kwenda Simba kuwa msaidizi wa Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye safu ya ulinzi hususan beki wa kushoto.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.