KIKOSI cha Yanga leo Septemba 30 kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya KMKM ya Zanzibar,utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo wa leo ni maalumu kwa ajili ya kujiweka sawa na mechi za Ligi Kuu Bara zinazoendelea ambapo kwa sasa ligi inaingia mzunguko wa tano.
Mchezo wa Yanga kwa mzunguko wa tano itakutana na Coastal Union ya Juma Mgunda Uwanja wa Mkapa, Oktoba 4 unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku.
Yanga mechi yao iliyopita ndani ya ligi wametoka kushinda bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri Morogoro wanakutana na Coastal Union iliyotoka kushinda bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania.
Coastal Union ipo nafasi ya 14 na pointi zake nne kibindoni huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 10 kibindoni.
Inakuwa ni mechi ya pili ya kimarafiki kwa Yanga kucheza ndani ya Uwanja wa Azam Complex ambapo kabla ya kuvaana na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba ilimenyana na Mlandege ya Zanzibar.
Kwenye mchezo huo Yanga ilishinda mabao 2-0 ambapo yalifungwa na Wazir Junior kwa mkwaju wa penalti na Tonombe Mukoko.