Home Uncategorized CHIRWA AITWA TIMU YA TAIFA MARA YA KWANZA

CHIRWA AITWA TIMU YA TAIFA MARA YA KWANZA

 

OBREY Chirwa,  mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha timu ya Azam FC amesema kuwa mwaka 2020 ni mara yake ya Kwanza kuitwa timu ya Taifa ya Zambia ya wakubwa katika maisha yake ya soka.


Chirwa ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Zambia itakayoanza kujiandaa na mashindano ya kimataifa. 


Nyota huyo ambaye msimu wa 2020/21 amekuwa wa Kwanza kufunga bao ndani ya Klabu ya Azam FC wakati wakishinda bao 1-0 mbele ya Polisi Tanzania hakuwa sehemu ya kikosi kilichoivaa Mbeya City kwa kuwa alipata majeraha Kwenye mchezo wao dhidi ya Coastal Union. 


Chirwa amesema:” Nilikuwa sijawahi kuitwa timu ya Taifa ya wakubwa zaidi ya zile za vijana ila msimu huu ni mara yangu ya kwanza kuitwa nimefurahi kweli na ninajiskia vizuri.”


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria thabit amesema kuwa wamepokea barua kutoka Chama cha Soka cha Mpira cha Zambia na Chirwa anatakiwa kuripoti kambini Oktoba 5 kwa ajili ya mechi tatu za kimataifa ambapo watacheza mechi dhidi ya Congo Oktoba 7, Kenya Oktoba 11 na Afrika Kusini Oktoba 13.

SOMA NA HII  BAADA YA BIRIANI LA SIMBA KULIWA,NENO LAO HILI HAPA