Home Uncategorized KAGERA SUGAR YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA

KAGERA SUGAR YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA

[the_ad id="25893"]


 UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho utakaowakutanisha mbele ya Yanga, Uwanja wa Kaitaba.


Kagera Sugar itamenyana na Yanga ikiwa imetoka kulazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Gwambina FC kwenye mchezo wao uliopita huku Yanga ikitoka kushinda bao 1-0 mbele ya Mbeya City.


Mecky Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa maandalizi yapo sawa na kila kitu kinakwenda vizuri.


“Kila kitu kipo sawa nasi tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ujao.Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi lakini tunahitaji kupata matokeo.


“Tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini tutapambana kupata matokeo chanya, mashabiki wajitokeze kuona ushindani utakavyokuwa pamoja na burudani,” amesema.


Mchezo huo utakaopigwa Septemba 19 utakuwa wa kwanza kwa Yanga kucheza nje ya Dar kwa msimu wa 2020/21 huku ukiwa ni wa pili kwa Kagera Sugar kucheza nyumbani.SOMA NA HII  HAO AZAM FC WAIPANIA POLISI TANZANIA KESHO UHURU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here