Home Uncategorized KUPOTEZA MBELE YA SPURS, LAMPARD HATA HAELEWI

KUPOTEZA MBELE YA SPURS, LAMPARD HATA HAELEWI


 FRANK Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa kupoteza kwake mbele ya Tottenham Hotspurs kumemvuruga kwa kuwa walianza kushinda ndani ya dakika 45 za mwanzo.

Mchezo huo wa Kombe la Carabao hatua ya 16 bora uliochezwa usiku wa kuamkia leo, Uwanja wa Tottenham Hotspur ulikuwa na ushindani mkubwa na dakika 90 zilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 jambo lililopelekea mshindi kupatikana kwa penalti.

Timo Werner dakika ya 19 alianza kufunga kwa Chelsea na lilisawazishwa dakika ya 83 na Erik Lamela ambapo kwenye penalti, Spurs inayonolewa na Jose Mourinho ilishinda penalti 5-4.Mason Mount alikosa penalti kwa upande wa Chelsea.

Lampard amesema kuwa wachezaji wake walionekana wamechoka kwenye mchezo huo jambo lililowafanya washindwe kuibuka na ushindi jumlajumla.

“Tulikiwa tunahitaji kubaki kwenye ushindani ila inaonekana wachezaji wangu walikuwa wamechoka,kwa hali ile ilikuwa ngumu kupata matokeo chanya na ilikuwa ni ngumu kwetu kupoteza kwa kuwa tulianza kushinda,” amesema.

SOMA NA HII  ISHU YA JEZI, YANGA YAIPIGA DONGO KIMTINDO SIMBA