KIGOGO wa soka kutoka Morocco, Wydad Casablanca, amekubali kapigika nje-ndani kwenye mtanange wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya bingwa wa kihistoria wa michuano hiyo National Al Ahly ya Misri.
Akiwa nyumbani Wydad alifungwa mabao 2-0, juma lililopita na usiku wa jana Ahly akaonyesha umwamba akiwa kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kushinda mabao 3-1.
Mabao ya Al Ahly yalifungwa na Marwan Mohsen dakika ya 5,Hussein El Shahat dakika ya 26 na Yasser Ibrahim dakika ya 56 na lile la Wydad lilifungwa na Zouhair El Moutaraji dakika ya 82.
Al Ahly wametinga fainali kwa jumla ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Wydad na sasa anamsubiri mshindi baina ya Zamalek ambaye anaoongoza mechi ya mkondo wa kwanza kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Raja.
Mtanange huo utachezwa Novemba Mosi, wakati fainali itachezwa Novemba 6 mwaka huu.
Haya ni mafanikio ya kocha mpya kutoka Afrika ya Kusini, Pitso Mosimane, ambaye amejiunga na Klabu hiyo hivi karibuni akitokea Mamelodi Sundowns.