Home Uncategorized FOUNTAIN GATE: MALENGO YETU KUSHIRIKI LIGI KUU BARA

FOUNTAIN GATE: MALENGO YETU KUSHIRIKI LIGI KUU BARA


 KWA miaka miwili mfululizo tangu 2018, Fountain Gate imefanikiwa kuwa miongoni mwa timu bora zilizofanikiwa kupanda daraja hadi kuweza kushiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu huu wa 2020/21 tangu kikosi kuanzishwa.

Katika msimu huu ndani ya kundi B, Fountain Gate imeweza kucheza michezo mitatu ambapo alicheza dhidi ya Alliance FC na kufunga mabao 3-0, Rhino Rangers 0-1 na Oktoba 24 Fountain Gate ilicheza dhidi ya Transit Camp na kuweza kufunga mabao 2-0 na kufanikiwa kuipa timu pointi tisa muhimu.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Juma Ayo amesema kuwa kinachowapa kasi ya mafanikio Fountain Gate ni lengo lao kuu la kutaka kupanda kwenye Ligi Kuu na uwezo mkubwa wa wachezaji waliokuwa nao katika kujielewa wakati wako uwanjani.

“Fountain Gate ilianzishwa mwaka 2018 na kiujumla, kinachoifanya Fountain Gate tuwe na kasi ya kupata mafanikio hadi kucheza msimu huu ni kwamba sisi tuna lengo kuu ya kutaka kushiriki katika Ligi Kuu Bara na ndio maana wachezaji wetu wanafanya juu chini katika kutimiza lengo hilo.

“Kwa upande wa wachezaji, naweza kujisifia kuwa Fountain Gate imejengwa na wachezaji wanaojielewa katika kutekeleza dhamira yao kuu pindi wako uwanjani. Wachezaji wetu pia wanaushirikiano,jambo ambalo limeipa tiketi kubwa sana timu hadi kupata ushindi uliokuwa nayo hadi sasa,” alisema Ayo.


SOMA NA HII  ULIMBOKA SASA BEGA KWA BEGA NA SALVATORY NDANI YA PAMBA SC