Home Uncategorized NAKIPA WATATU STARS WAMPASUA KICHWA KOCHA, REKODI ZAO BALAA

NAKIPA WATATU STARS WAMPASUA KICHWA KOCHA, REKODI ZAO BALAA


OKTOBA 2, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije alitangaza  kikosi ambacho kitaingia kambini Oktoba 5 kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi, vita kubwa inaonekana kwenye upande wa mlinda mlango.

Kwenye jumla ya wachezaji 25 waliochaguliwa, wameitwa makipa watatu kutoka timu tatu tofauti ambao ni Metacha Mnata kutoka Yanga, Aishi Manula kutoka Simba na David Kisu kutoka Azam FC.

Rekodi zinaonyesha kuwa ndani ya Ligi Kuu Bara, makipa hao wote ni namba moja ndani ya timu zao walizotoka ambapo ni mchezaji mmoja wa Yanga, Mnata kwenye mechi nne zile za mzunguko wa kwanza alikosa mechi moja mbele ya Tanzania Prisons.

Kisu na Manula ambao wamekaa langoni kwenye mechi zote tano, wao vita yao ni kwenye kusepa na ‘CleanSheet’ ambapo, Kisu ameonekana ni balaa akiwa nazo nne huku Manula akiwa nazo tatu na Mnata kwenye mechi zake nne alizoanza hakutunguliwa.

Mechi za Kisu ilikuwa :Azam 0-1 Polisi Tanzania, Azam 2-0 Coastal Union,Mbeya City 0-1 Azam FC na Tanzania Prisons 0-1 Azam FC, Azam 4-2 Kagera Sugar.


 Manula ilikuwa Ihefu 1-2 Simba, Mtibwa Sugar 1-1 Simba, Simba 4-0 Biashara United na Simba 3-0 Gwambina, JKT Tanzania 0-4 Simba.


Mnata ilikuwa Yanga 1-0 Mbeya City, Kagera Sugar 0-1 Yanga na Mtibwa Sugar 0-1 Yanga.Yanga 3-0 Coastal Union.

Kwa rekodi zao namna zilivyo Ndayiragije lazima kichwa kivurugike kwanza kabla ya kujua nani atakuwa ni namba moja Oktoba 11 wakati Stars itakapomenyana na Burundi kwenye mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA  kwa kuwa kila mmoja ana uwezo wake na uzoefu ndani ya uwanja.

SOMA NA HII  MWINYI ZAHERA AIPA USHINDI YANGA MBELE YA SIMBA, JULAI 12