Home Uncategorized NYOTA AZAM FC ATIMKIA ISRAEL

NYOTA AZAM FC ATIMKIA ISRAEL

 

KIUNGO Novatus Dismas ameuzwa kwenda Klabu ya Macabi Tel Aviv ya Israel kutoka Klabu ya Azam FC.


Nyota huyo mwenye tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa msimu wa 2019/20 dili lake limejibu baada ya kufanya vizuri majaribio yake.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa majaribio yake timu ya wakubwa alifaulu jambo ambalo limewafanya mabosi wa Macabi Tel Aviv kurudi mezani na kupewa kijana huyo raia wa Tanzania.


“Alifanya vizuri majaribio ya kwanza kwa timu ya vijana na alipokwenda timu ya vijana aliweza kufanya vizuri na alipopata nafasi kwenye timu kubwa aliweza kufanya vizuri pia.


“Tumefikiana makubaliano mazuri na timu hiyo hivyo kwa sasa atakuwa ni mali ya Macabi Tel Aviv hivyo kikubwa ni kuona anaweza kufanya vizuri,” amesema.

SOMA NA HII  MANCHESTER UNITED WAPEWA UBINGWA WA LIGI KUU ENGLAND