DIEGO Maradona legendi wa zamani wa timu ya Taifa ya Argentina ameripotiwa kupelekwa hospitali kutokana na kutokuwa fiti kwa afya huku wakigoma kuweka wazi kama anasumbuliwa na Corona.
Maradona, mwenye miaka 60, alipelekwa hospitali kufanyiwa vipimo baada ya kujihisi vibaya kutokana na afya yake kutokuwa kwenye ubora.
Legendi huyo atakumbukwa kwa uwezo wake ndani ya uwanja pamoja na vituko vyake ambapo akiwa na timu ya Taifa ya Argenitina alikiongoza kikosi hicho kutwaa taji la Kombe la Dunia mwaka 1986 na anatajwa kuwa mchezaji bora wa muda wote ndani ya Taifa la Argentina.
Daktari wa Maradona, Leopoldo Luque amesema kuwa nyota huyo alijiskia vibaya ghafla jambo lililofanya afanyiwe vipimo ili kujua kinachomsumbua gwiji huyo.
“Amekuwa akijihisi vibaya ila ninaamini kwamba baada ya kufanyiwa vipimo kila kitu kitawekwa wazi na tatizo lake litajulikana, hayupo sawa kiafya hayupo sawa labda baada ya muda tutajua mambo yatakuaje,” amesema.
.