Home Uncategorized HESABU ZA SIMBA KWA SASA NI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

HESABU ZA SIMBA KWA SASA NI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

 


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wameweka wazi kuwa hesabu zao kubwa kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.


Msimu uliopita Simba ilipokuwa chini ya Patrick Aussems iliishia hatua ya awali kwa kutolewa na UD Songo kwa faida ya bao la ugenini jambo ambalo lilisababisha kibarua cha kocha huyo ambaye aliifikisha hatua ya robo fainali timu hiyo kuota nyasi.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hesabu kubwa kwa sasa ndani ya timu hiyo ni kuweza kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.


“Tunakazi kubwa ya kufanya kimataifa hasa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo tuna amini kwamba wachezaji pamoja na benchi la ufundi watafanya kazi kubwa kufikia malengo.

“Mashabiki watupe sapoti katika hili kwani kufikia mbali huko lazima tuwe nguvu moja na hii ni sera ya Simba na ipo kwenye nembo yetu hivyo kazi kubwa ni kufanya vizuri kimataifa,” amesema.

 Simba itakutana na Plateu United ya Nigeria mchezo unaotarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 27-29  na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 4-6 Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  MAGORI AACHIA NGAZI RASMI SIMBA, CEO MPYA KUTOKA AFRIKA KUSINI ATANGAZWA