Uncategorized

KOCHA UFARANSA: POGBA HANA FURAHA NDANI YA MANCHESTER UNITED

admin November 12, 2020 12:47 pm


 KOCHA wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amesema kiungo wa Manchester United, Paul Pogba, hana furaha na nafasi anayochezeshwa kwenye timu hiyo na kumfanya ashindwe kuwika msimu huu.

 

Deschamps amemkingia kifua kiungo huyo, kuwa alikuwa majeruhi kwa muda mrefu hivyo anahitaji muda wa kucheza ili kurejesha makali yake aliyokuwa nayo hapo awali.


 United inaonekana kukosa uwiano pindi wanapocheza na Bruno Fernandez, hivyo kumfanya Pogba kuanzia kwenye benchi.

 

“Pogba hana furaha ndani ya United kutokana na nafasi ambayo anachezeshwa kutokuwa yake ila nina amini kwamba bado ana uwezo mkubwa na akiaminiwa ataonyesha yale aliyonayo na watafurahi wenyewe,” amesema.

YANGA YAIPIGA KIJEMBE KIMTINDO SIMBA ISHU YA CHAMA MZUNGUKO WA 10 KUNA MAMBO YA KUJIFUNZA, LIGI DARAJA LA KWANZA ISIPEWE KISOGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply