Home Uncategorized YANGA WAINGILIA KATI DILI LA MUKOKO KUIBUKIA SIMBA

YANGA WAINGILIA KATI DILI LA MUKOKO KUIBUKIA SIMBA


 MABOSI wa Yanga wameweka wazi kuwa watamuongezea mkataba kiungo bora ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 kwa mwezi Oktoba, Tonombe Mukoko anayetajwa kuingia anga za Simba.


Ikiwa watamuongeza mkataba nyota huyo watazima ndoto za watani zao wa jadi kuipata saini ya kiungo huyo ambaye ni miongoni mwa wanaofanya vizuri kwa msimu wa 2020/21 na kuingilia kati dili hilo kibabe.


Mukoko aliibuka ndani ya Yanga kwenye dirisha kubwa akitokea Klabu ya AS Vita ya Congo pamoja na mwenzake Tuisila Kisinda ambao kwa pamoja wamekuwa na pacha matata ndani ya uwanja.


Kwa msimu huu pacha yao imekuwa na moto ambapo kwenye Dar Dabi, Kisinda alisababisha penalti iliyofungwa na Michael Sarpong huku Mukoko akisepa na tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo ikiwa ni dabi yao ya kwanza.


Kutokana na ubora wa Mukoko kuweza kumzima kiungo ghali Bongo, Clatous Chama wa Simba, watani zao wa jadi walikuwa wanatajwa kumuweka kwenye hesabu nyota huyo jambo ambalo limewashtua mabosi wa Yanga.


Kupitia kwa Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga na walihusika kwenye usajili wa nyota huyo umeweka wazi kwamba utamuongezea mkataba nyota huyo.


“Mukoko ana mkataba wa miaka miwili yeye na Kisinda lakini muda wowote wanaweza kuongezewa mkataba kwa kuwa kuna kipengele cha kumuongezea mkataba kwenye ule mkataba ambao tuliusaini wakati ule na AS Vita,” amesema.



SOMA NA HII  WINGA MZAMBIA MAMBO SAFI YANGA