UONGOZI wa Yanga umetangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi wa Hostel za timu hiyo ambazo zitajengwa Kigamboni pamoja na uwanja wa mazoezi.
Taarifa rasmi ambayo imetolewa na Yanga imeeleza kuwa mchakato huo umefika hapo baada ya mipango kwenda sawa ndani ya Yanga.
Kwa sasa Yanga inawaalika wale wote ambao wana uwezo wa kusimamia na kubuni mradi huo ambao utajengwa maeneo ya Kigamboni kwa mpango kazi wa fedha za msimu wa 2020/21.
Malengo makubwa ya Yanga ni kuweza kutimiza yale ambayo walianza kuyafikiria awali kwa kuwa mwanzo ujenzi huo ulianza ukiwa ni wazo na sasa wanahitaji kukamilisha wazo hilo kwa kulitendea kazi.
Zabuni (tender) ya ujenzi wa Hosteli na Uwanja wa mazoezi wa klabu eneo la Kigamboni kwa sasa ipo wazi kwa wale wenye vigezo.