DAKIKA 270 ulimwengu wa michezo umeshuhudia matokeo ya saresare kwa timu zote zilizoshuka Uwanja wa Mkapa kwa kupata matokeo yanayofanana kwenye mechi tatu mfululizo.
Hakuna timu ambayo imesepa na pointi tatu kwa mpinzani wake kwenye mechi tatu zilichezwa uwanjani matokeo yamekuwa pacha ndani ya dakika 270 kwa timu zote kupata sare ya kufungana bao 1-1.
Novemba 7, Yanga 1-1 Simba, mchezo huu wa ligi mabao yalifungwa na Michael Sarpong kwa mkwaju wa penalti upande wa Yanga na dakika ya 31 na kwa Simba Joash Onyango dakika ya 86 kwa mpira wa adhabu ya kona iliyopigwa na Luis Miquissone.
Novemba 17, Tanzania 1-1 Tunisia, kwa Tunisia, bao lilifungwa na Saif-Eddine Khaoui dakika ya 11 na kwa Tanzania, Feisal Salum alipachika bao dakika ya 47.
Novemba 22, Yanga 1-1 Namungo. Kwenye mchezo huu wa Ligi Kuu Bara raundi ya 11, Yanga ilianza kufunga dakika ya 13 kupitia kwa Carlos Carlinhos na lile la Namungo lilipachikwa na Stephen Sey dakika ya 16.