HEMED Morroco Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa watapambana kesho kwa hali na mali kupata matokeo chanya mbele ya Al Rabita FC ya Sudan Kusini kwenye mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho.
Tayari wapinzani hao wa Namungo FC wameshatua Dar tangu Novemba 25 na kuweka ngome yao mitaa ya Karume, Ilala.
Kesho watashuka uwanjani saa 1:00 kwenye mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Morroco ambaye amebeba mikoba ya Hitimana Thiery aliyekuwa na timu msimu uliopita na kuiongoza kwenye mechi 10 za ligi msimu huu kabla ya kufutwa kazi na mikoba yake kuchukua Morroco.
“Maandalizi yapo vizuri na imani yetu ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya kwenye mchezo wetu wa kwanza.
“Tunatambua kwamba tutakuwa nyumbani hivyo ni lazima tupambane kupata matokeo chanya katika hilo wachezaji wanajua nini tunahitaji na Tanzania inahitaji kuona tunapata ushindi.
“Kwa hapa ninaona kwamba hatutawaangusha Watanzania tunahitaji kupata matokeo hakuna jambo lingine ili tukienda ugenini tusiwe na presha kubwa,” amesema.