Home Uncategorized SIMBA :HAIKUWA MIPANGO YETU KUPATA SARE MBELE YA YANGA

SIMBA :HAIKUWA MIPANGO YETU KUPATA SARE MBELE YA YANGA


 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kupata sare ya kufungana baoa 1-1 dhidi ya Yanga jana Novemba 7 haikuwa kwenye mpango wake wa kazi.


Simba wakiwa ugenini walikubali kugawana pointi mojamoja na watani zao wa jadi Yanga ambao walikuwa ni wenyeji kwenye mchezo huo.

Michael Sarpong alianza kupeleka maumivu kwa Simba dakika ya 31 kwa mkwaju wa penalti na Joash Onyango aliweka mzani sawa dakika ya 86.


Sven mwenye kibarua cha kutetea taji la Ligi Kuu Bara amesema kuwa ilikuwa ngumu kuamini kwamba ameambulia sare kutokana na maandalizi waliyofanya.


“Tulikuwa na maandalizi mazuri licha ya kwamba tuliwakosa wachezaji wetu wengine ikiwa ni pamoja na Meddie Kagere na Chris Mugalu.


“Yote ambayo yametokea tunayachukua na tutayafanyia kazi kwa ajili ya mechi zijazo, haikuwa mpango wetu kuambulia sare tulikuwa tunahitaji ushindi,” amesema.


Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20 inaachwa na Yanga kwa pointi nne kwa kuwa imefikisha pointi 24 ikiwa nafasi ya pili zote zimecheza mechi 10 na kinara ni Azam FC mwenye pointi 25.

SOMA NA HII  SIMBA WABADILI GIA ANGANI KISA MPIRA HUU