Home Uncategorized SIMBA KUVUTA MAJEMBE YA KAZI, WATATU WAPO KWENYE ORODHA

SIMBA KUVUTA MAJEMBE YA KAZI, WATATU WAPO KWENYE ORODHA

 


UONGOZI wa Simba umeweka bayana kuwa utafanya usajili wa kushtua kwenye dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15.


Simba chini ya Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck ina kibarua cha kupeperusha bendera ya Taifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mchezo wa awali itakuwa ugenini mbele ya Plateau United ya Nigeria.


Habari zinaeleza kuwa mpango mkubwa wa Simba ni kufanya mabresho kwenye sehemu kuu mbili ikiwa ni ile ya ulinzi pamoja na kiungo.

Majina ya pacha mbili zinazokipiga ndani ya Yanga, Tuisila Kisinda na Tonombe Mukoko ambao walisaini dili la miaka miwili ndani ya Yanga wakitokea Klabu ya AS Vita yanatajwa kuwa kwenye orodha ya nyota waliopo kwenye rada.


Pia jina la kiungo mkabaji, James Kotei ambaye alikuwa ndani ya Simba na alicheza kwa mafanikio anatajwa kurejeshwa ndani ya kikosi hicho.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ikitokea wakahitaji kufanya usajili basi hakuna kitachoshindikana kwa mchezaji watakayemtaka.


“Simba tukiamua jambo letu hatushindwi ila kwa sasa tunasubiri wakati wa usajili ufike tutafanya mambo makubwa na wengi watashtuka, watatikisika kwa namna ya vile ambavyo tutafanya,” amesema.


Kuhusu nyota hao wa Yanga kutajwa kuibukia Simba, Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa klabu hiyo ameweka bayana kwamba nyota hao wana mikataba.


“Kuhusu Mukoko,(Tonombe) mashabiki wasiwe na mashaka ana mkataba wa miaka miwili ambao anautumikia kwa sasa hivyo wasiwe na presha,” amesema.

SOMA NA HII  NAMUNGO YAZITAKA POINTI TATU ZA KAGERA SUGAR