Home Uncategorized SIMBA: TUNACHUKUA TENA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

SIMBA: TUNACHUKUA TENA UBINGWA WA LIGI KUU BARA


 SHOMARI Kapombe, beki wa kulia mzawa ndani ya Simba ambaye pia jina lake limetajwa kwenye majina ya wachezaji 27 kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije amesema kuwa wanaamini watatwaa ubingwa wa ligi.

Simba ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ambao waliutwaa msimu wa 2019/20 baada ya kucheza mechi 38 na kufikisha jumla ya pointi 88.


Baada ya jana Novemba 7 kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1inabaki nafasi ya tatu na pointi 20.



Kwenye mechi zote 10 ambazo Simba ilikuwa imecheza, Kapombe ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji na alitumia jumla ya dakika 824.

Msimu uliopita wakati Simba ikitupia jumla ya mabao 78 alihusika kwenye mabao sita ambapo alitengeneza jumla ya pasi sita za mwisho zilizoleta mabao.

Kapombe amesema:”Tuna kazi kubwa ya kufanya kwetu sisi wachezaji kutimiza majukumu yetu ndani ya uwanja, lengo letu ni kuona tunatwaa ubingwa na ili hilo liwezekane ni lazima tushinde mechi zetu.

“Kikubwa ninawaambia mashabiki waendelee kutupa sapoti katika kazi yetu kwani uwepo wao uwanjani unatuongezea nguvu,” amesema.

SOMA NA HII  YANGA WALAMBA SHAVU KUTOKA SHIRIKA LA BIMA LA NIC