Home Uncategorized MABADILIKO NDANI YA YANGA MCHAKATO WAFIKA PATAMU

MABADILIKO NDANI YA YANGA MCHAKATO WAFIKA PATAMU

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mchakato mzima wa kuelekea kwenye mfumo wa mabadiliko ya timu hiyo asilimia 100 umesimamiwa na Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga na mpaka hatua ambayo wamefika kwa sasa ni kubwa.


Hivi karibuni Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka kampuni ya GSM Injinia. Hersi Said na Alvaro Paya mwakilishi wa La Liga walikwea pipa kuelekea Hispania kwa ajili ya kukabidhiwa rasmi rasimu ya awali ya uendeshwaji wa klabu.


Akizungumza na Waandishi wa Habari muda huu Hotel ya Serena, Mwenyekiti wa Yanga, Dr. Mshindo Msola amesema kuwa kuna karatasi 400 ambazo zimezungumza kuhusu mchakato huo ambao utaleta mabadiliko ndani ya Yanga kwa kufuata sheria za Serikali.


Msola ameongeza kuwa walipaswa kufanya mkutano hivi karibuni ila walighairii kwa ajili ya mchakato huo ambapo leo makabidhiano ya rasmu hiyo imefanyika huku uongozi ukiwa umeanza kuandaa mpango kazi kwa ajili ya mkutano mkuu utakaoitishwa  hivi karibuni


Mshauri kwenye masuala ya mabadiliko, Senzo Mbatha amesema kuwa anaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa na watafikia malengo ambayo wanayahitaji.

SOMA NA HII  SINGIDA FG HALI SIO SHWARI LIGI KUU