Home Uncategorized YANGA YAFICHUA KILICHOIPONZA RUVU SHOOTING

YANGA YAFICHUA KILICHOIPONZA RUVU SHOOTING


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakifuata maelekezo ndani ya uwanja jambo linalowafanya wapate ushindi kwenye mechi zao huku akiweka wazi kuwa makosa waliyalofanya wapinzani wake yalikuwa faida kwao.


Jana, Desemba 6 Yanga ilisepa na pointi tatu muhimu Uwanja wa Mkapa kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting na kuifanya ijikite kileleni ikiwa na pointi 31.


Ikiwa imecheza jumla ya mechi 14 ndani ya Ligi Kuu Bara haijapoteza mchezo hata mmoja ndani ya dakika 90.


Kaze amesema:”Wachezaji wangu wanafuata maelekezo ndani ya uwanja jambo linalowafanya wanapata matokeo chanya hii ni furaha kwangu na kwao pia.


“Kikubwa ambacho tunakitazama ni pointi tatu muhimu kisha baada ya kuzikusanya hizi tunatazama kipi tufanye ili kuwa bora zaidi kwa kuboresha makosa.


“Mashabiki pia wamekuwa wakitupa sapoti hii ni furaha pia inatufanya tuzidi kupambana ndani ya uwanja,” amesema. 


Baada ya kushinda mchezo wake wa Kwanza kwa mwezi Desemba kigongo kinachofuata ni dhidi ya Mwadui FC.

SOMA NA HII  ALIYEMBANA MEDDIE KAGERE ALIPEWA MBINU NA SIMBA WENYEWE