NAMUNGO FC kimataifa
BAADA ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Rabita ya Sudan Kusini uliotarajiwa kuchezwa Desemba 6 kufutwa na Shirikisho la Soka Afrika,(Caf) timu hiyo imesonga mbele na inakutana na timu ya Sudan.
Namungo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morroco mchezo wa awali ilishinda mabao 3-0 , Uwanja wa Azam Complex na mchezo wa marudio ulitarajiwa kuchezwa Azam Complex.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imesema kuwa Namungo imesonga mbele hatua ya pili ya mchujo Kombe la Shirikisho na itacheza na El Hilal Obeid ya Sudan.
Mchezo wa awali unatarajiwa kuchezwa Desemba 23 na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Kati ya Sudan Januari 5 na 6.