Home Uncategorized SIMBA KAZINI KESHO KUSAKA POINTI TATU MUHIMU DHIDI YA KMC

SIMBA KAZINI KESHO KUSAKA POINTI TATU MUHIMU DHIDI YA KMC

BAADA ya kumaliza kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine Mbeya kwa kushinda bao 1-0 kesho ina kazi ya kusaka pointi nyingine mbele ya KMC.


Tayari kikosi cha Simba kinachonolewa  na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kimeshatia timu Dar es Salaam, jana Desemba 14 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara. 


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kuwa na mwendo mzuri ndani ya uwanja zikiwa kwenye viwanja vya Dar.

KMC imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro itaingia ndani ya uwanja ikiwa na hasira za kulipa kisasi cha kupoteza.


Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na wanahitaji pointi tatu muhimu.


Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anaamini utakuwa mchezo mgumu ila anahitaji pointi tatu muhimu.

SOMA NA HII  SIMBA KUIFUATA KMC KWA TAHADHARI HII LEO