GABRIEL Jesus nyota wa Manchester City aliwapoteza jumla kwenye ramani wapinzani wake Arsenal baada ya kupachika bao la mapema kabisa dakika ya 3.
Jitihada za Arsenal ya Mikel Arteta kupindua meza Uwanja wa Emirates ziligonga mwamba kwa kuwa ni Alexandre Lacazette dakika ya 31 aliandika bao la kufuta machozi.
Bao hilo la kuweka mzani sawa liliongeza hasira kwa Manchester City ambao waliongeza misumari mitatu kwa Arsenal kipindi cha pili na kusepa na pointi tatu zote mazima.
Kwa Manchester City wambao walicheka na nyavu ni Riyad Mahrez dk 54, Phil Foden dk 59 na Aymeric Laporte dk 73.
Ushindi huo unaifanya Manchester City kuwa nafasi ya 8 na pointi 23 huku Arsenal ikiwa nafasi ya 15 na pointi 14.
Arsenal imekuwa kwenye mwendo mbovu jambo ambalo linampasua kichwa Arteta ambaye amesema kuwa anawaonea huruma wachezaji wake.