Home Uncategorized KIPIGO KUTOKA KWA WAZIMBABWE CHASEPA NA FURAHA YA MBELGIJI WA SIMBA

KIPIGO KUTOKA KWA WAZIMBABWE CHASEPA NA FURAHA YA MBELGIJI WA SIMBA


 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, raia wa Ubegiji amesema kuwa hajafurahisha na matokeo aliyoyapata kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ulikamilika kwa dakika 90 kwa mabingwa hao watetzi wa Ligi Kuu Bara kushindwa kuweka mzani sawa.


Licha ya kufungwa dakika ya 17 na Perfect Likwende kutokana na mabeki kuzidiwa ujanja na nyota huyo wa FC Platinum ngoma ilikamilika kwa Simba kupoteza mchezo wa kwanza.


Ina kazi yakufanya kwenye mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Januari 5 kwa kutakiwa kuwa na chaguo moja la kushinda mabazo zaidi ya mawili ikikwama hapo itakuwa imetolewa jumlajumla kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.


Sven amesema kuwa wachezaji wake hawakuwa makini jambo ambalo litawafanya wawe makini kwenye mchezo wa marudio


“Tunapaswa kuwa makini zaidi kwenye mchezo wa marudio kwa sababu tulistahili kushinda kwenye mchezo wetu ambao tulitawala kwa asilimia kubwa.

“Sijafurahishwa na matokeo ambayo tumeyapata ugenini hivyo tuna kazi ya kufanya mchezo wetu wa nyumbani,” .


Mchezo wa jana Simba ilikosa huduma ya nyota wake John Bocco ambaye anasumbuliwa na majeraha huku Aishi Manula ambaye taarifa ya awali ilieleza kuwa hayupo fiti aliweza kukaa langoni.

SOMA NA HII  MESSI ATAJWA KUIBUKIA INTER MILAN