KOCHA Mkuu wa Biashara United, Francis Baraza amesema kuwa atatumia muda huu wa dirisha dogo kufuma kikosi bora kitakachorejea na ushindani ndani ya uwanja.
Baraza amekuwa na mwendo mzuri ndani ya Biashara United kwa msimu huu wa 2020/21 ambapo amekiongoza kikosi chake kucheza jumla ya mechi 17 na kujikusanyia pointi 26.
Kipo ndani ya tano bora ambapo kimeshinda jumla ya mechi saba, sare tano sawa na zile ambazo walipoteza ndani ya Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Saleh Jembe, Baraza amesema kuwa wamejipanga kufanya vizuri ndani ya ligi kwa kuboresha kikosi kwenye dirisha dogo ambalo limefunguliwa Desemba 16.
“Tumejipanga kuboresha kikosi kwa wakati huu wa dirisha dogo, ninaona kwamba vijana wanahitaji kuongezewa nguvu hasa kwenye safu ya ushambuliaji na ulinzi.
“Ukweli ni kwamba ninapenda namna ambavyo wanashika maelekezo na kufanya kile ambacho ninawaambia jambo ambalo linanifanya niamini kwamba tukipata wachezaji wenye uzoefu basi tutaendelea kuwa bora.
“Kila timu ndani ya uwanja inasaka ushindi, nasi pia tunaingia uwanjani tukihitaji ushindi kwa sababu muhimu kupata pointi tatu,” .