Home Uncategorized SABABU ZA MKUDE KUCHIMBISHWA SIMBA ZATAJWA

SABABU ZA MKUDE KUCHIMBISHWA SIMBA ZATAJWA


 IMEELEZWA kuwa sababu ya nyota wa kikosi cha Simba, Jonas Mkude kusimamishwa na mabosi wa timu hiyo ni mfululizo wa makosa ya mara kwa mara ikiwa ni pamoja na unywaji pombe kupitiliza.

Kiungo huyo mkabaji Desemba 28 amesimamishwa na Simba huku akitarajiwa kupelekwa kamati ya nidhamu kujibu shutuma zinazomkabili.

Ndani ya Ligi Kuu Bara chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kikosi hicho kikiwa kimecheza jumla ya mechi 14 yeye amecheza mechi 10 akikosekana kwenye mechi nne.

Katika mechi hizo 10 alizocheza moja alianzia benchi huku tisa akianza kikosi cha kwanza ndani ya timu hiyo inayopambana kutetea taji la ligi

Habari zinaeleza kuwa nyota huyo alikunywa kupita kiasi kabla ya timu yake kuvaana na FC Platinum ya Zimbabwe wakati Simba ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

“Mkude amekuwa na tabia za kunywa kupita kiasi hata kabla ya mechi ngumu na muhimu, licha ya kuonywa amekuwa akirudia kufanya makosa hayo hata nchini Nigeria alifanya hivyo hata Zimbabwe.

“Pia amekuwa ni mwenye kununa kila mara kwa wachezaji wenzake na hata viongozi hivyo kwa sasa madai yake yanafanyiwa uchunguzi na yeye ataitwa kujibu,” ilieleza taarifa hiyo.


Simba leo itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Ihefu na Januari 6 ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya FC Platinum ya Zimbabwe.

SOMA NA HII  MANE AINGIA ANGA ZA MADRID