Home Uncategorized SAKATA LA MKUDE NA SIMBA LIMEFIKIA HAPA

SAKATA LA MKUDE NA SIMBA LIMEFIKIA HAPA

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa suala la kiungo wa Simba, Jonas Mkude litatolewa ufafanuzi wiki ijayo na kuwataka mashabiki watulie.


Mkude alisimamishwa na Simba Desemba 28 kwa kile kilichoelezwa kwamba ni utovu wa nidhamu na anafanyiwa uchunguzi na Kamati ya Nidhamu ambayo itatoa hukumu yake hivi karibuni.


Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara leo dhidi ya Ihefu FC wakati Simba ikishinda mabao 4-0 hakuwa sehemu ya kikosi cha Sven Vandenbroeck.


Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa suala hilo linafanyiwa uchunguzi na majibu yatatolewa.


“Mashabiki wasiwe na mashaka suala la Jonas Mkude lipo kwenye kamati ya nidhamu litatolewa wiki ijayo, mashabiki wasiwe na mashaka kila kitu kitakwenda sawa,” amesema.

SOMA NA HII  MBELGIJI WA SIMBA AFICHUA SIRI ZA CHAMA NA SHEVA